UHAKIKI WA RIWAYA YA JOKA LA MDIMU (2024)

Jina la Riwaya: JOKA LA MDIMUMwamfcsbi: ABDALA J.SAFARIMchapisha: JK HUDA PUBLISHERSMwaka: 2007

UTANGULIZI

Riwaya ya Joka la Mdimu ni riwaya ambayo inaakisi vizuri matatizo ya kiuchumi ya miaka ya themanini nchini Tanzania. Riwaya hii inaaksi tu, haihakiki, hali ya maisha katika kipindi cha dhiki ya ukosefu wa bidhaa muhimu kama vile nguo, chakula, mafuta, spea za mashine, n.k. Wakati huu wa dhiki watu wengine wanateseka na kuumia, kuna wengine wachache wanaotumia nafasi zao kuchuma kadri wanavyoweza, hasa kwa njia haramu. Katika Joka la Mdimu vilevile wengine wanaotanafusi katika maisha yao wanakuwa hivyo kwa kupitia njia zisizo halali.Mwandishi wa ]oka la Mdimu anaonekana kuwa alifanya uchunguzi mkali kabla ya kuandika riwaya yake. Hii inajidhihirisha kutokana na jinsi anavyopenya katika nafsi za nje na ndani za wahusika wake, akiwapatia lugha, mavazi, vyakula, tabia na mazingira yanayochukuwana nao na ujumi wa makundi yao, na hivyo kuhalisisha uhusika wao kwa namna inavyomlidhisha msomaji. Kwa jinsi riwaya hii inavyoaridhia vizuri matukio ya kipindi cha mwanzo cha miaka themanini katika Tanzania inabeba sifa ya kuwa ni riwaya kiistiara.

PITIO LA KITABU

Sehemu ya kwanza: Mindule

Amani ambaye ni dereva wa taxi anatafakari kitandani namna ya kupata mafuta. Anaondoa gari yake ya Zalpher 6 kwake na kusaka mafuta na wateja. Mafuta ni shida kuyapata na yanapatikana kwa magendo.Ugumu wa maisha unawafanya vijana wa kike kujitumbukiza kwenye biashara ya ukahaba na kufungua madangulo ilimradi wapate fedha za kujikimu maisha.

Sehemu ya mbili: Tino

Maisha ya wakazi wananchi wa Sega kwa kiasi kikubwa ni duni. Huko ndiko alikoishi Tino, mvuta kwama. Mvua kubwa kubwa inanyesha na kusababisha mafuriko. Tino anamuokoa bibi na mafuriko, anaendelea na shughuli zake za kukokota kwama na kubeba mizigo. Tunahadhithiwa kuhusu watu kukataa kulima kahawa kwani ujka wake ni mdogo. Hali ya chakula, mafuta na fedha za kigeni ni mbaya.

Sehemuya tatu: Jinja Maloni

Jinja Maloni analetewa taarifa kuhusu kifo cha rafiki yake mpenzi Omar Mahafudh. Anaombwa kwenda kuchimba kaburi. Marehemu alikuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo. Jinja alikuwa mzibua vyoo pia.Jinja Maloni anamuokoa mwanamke aliyekuwa anabakwa na wanaume wawili. Anaamua kupigana na wale wahuni ili kumuokoa yule mwanamke. Anafanikiwa kumuokoa na ku*msindikiza nyumbani kwao.

Sehemu ya nne: Sega

Wakazi wengi wa Sega ni waislamu. Tino naye ni mmoja wa waislamu. Ni mpenzi wa timu ya Sega Warriors. Alichezea timu hii licha ya umri wake kusonga. Siku ya mchezo kati ya Sega Warriors na City Devils ilimpa hofu sana Tino. Viongozi wanakabidhiwa dawa ya kuleta ushindi toka kwa Sangona. Katika mchezo, huo, Sega walipata ushindi uliotokana na bao pekee lililofungwa na Tino. Amani anaamua kuwaandalia sherehe ya kuwapongeza Tino na Zitto. Wanakunywa na kula ukumbini G.V. Tino alirudi nyumbani baada ya mkesha. Alikutana na familia yake ikiwa imerudi toka safarini. Tino anabeza sherehe za uhuru wa nchi. Tino anafanya maandalizi ya Iddi El Fitri.

Sehemu ya Tano: Boko

Amani anakwenda posta kuchukua barua. Anampatia Tino telegramu yake. Telegramu ilimtaarifu kuhusu kuumwa kwa Cheche. Tino anasafiri kumwona Cheche. Cheche alikuwa ameumia vibaya na amelazwa katika hospitali.

Sehemu ya Sita: Brown Kwacha

Amani anaendesha gari kuelekea hazina. Ndani ya gari kuna tajiri aitwae SHIRAZ BHANJ. Bhanj alikuwa anataka kumuona Mkurugenzi wa fedha za kigeni aliyeitwa BROWN KWACHA. Brown alipenda anasa hususani ufusika na uasherati. Brown Kwacha anafanya biashara ya nyara za Serikali. Brown anakaidi kuwahudumia wageni wengine isipokuwa kwa wasichana kama vile Leila na Josephine.Brown Kwacha ananunua viwanja 2 vya kujenga nyumba. Anafanya sherehe za kuzindua nyumba. Siri ya mahusiano mabaya kati ya Brown na mkewe inaelezwa.

Sehemu ya Saba: Kwale

Brown Kwacha anatoa udhuru wa kutokuwepo kazini. Anajiandaa kwa safari ya kwenda mbuga ya wanyama na Leila. Walienda hifadhi ya taifa ya KWALE. Anapanga mipango na maharamia kumletea nyara (pembe za ndovu).

Sehemu ya Nane: Dakta Mikwala

Hospitalini Mindule, amelazwa Cheche. Afya yake inazorota, wazazi wanajawa na simanzi. Mama yake analia, Cheche anakata tamaa ya kupona, anasema, "Mimi siponi baba" (uk. 123) Tino anampa matumaini ya kupona mwanae Cheche. Daktari Denis Kaya wa hospitali ya Manga anamshauri Tino ampeleke hospitali ya Glasgow, Uingereza. Tino na Amani wanapanga namna ya kumpata Daktari bingwa wa mifupa. Daktari Mikwala anapendekeza Cheche apelekwe Glasgow — Uingereza kwa matibabu zaidi.

Sehemu ya Tisa: Cheche

Amani anakwenda ofisi ya hazina kuonana na Brown Kwacha kuhusu uwezekano wa kupata fedha za kigeni za kumtibia Cheche nje ya nchi. Taarifa kutoka kwa Brown Kwacha zinamsononesha Tino na anaonekana kukata tamaa kuambiwa kuwa zinatakiwa laki tatu na pia kulipia nusu ya gharama za matibabu ambazo zinagharimu kiasi cha milioni tano. Nyumba mbili za Kashogi zinaungua, majirani na gari la zimamoto wanasaidia bila mafanikio.Amani ananunua bastola kwa askarijeshi mmoja. Tino na Amani wanatumia bastola hiyo katika tukio la wizi katika benki. Wanaiba milioni 20 kwa kutumia gari aina Peugeot 504. Fedha hizo zinatumika kumtibia Cheche.

Sehemu ya Kumi: Moto

Brown Kwacha analazwa katika hospitali ya rufani jijini Mindule kufuatia kuziba kwa tundu la mkojo kwa siku mbili. Brown Kwacha anapata mstuko baada ya kusoma gazeti la 'Time' lenye habari za wabunge kudai maelezo kuhusu meli ya mafuta. Daktari anamshauri Kwacha afanyiwe upasuaji katika kibofu cha mkojo.Waziri wa fedha anafika nyumbani kwa Brown Kwacha kupata mahesabu ya matumizi ya fedha za kigeni, Brown Kwacha anamuahidi Waziri kuwa atawatuma vijana walete hayo mahesabu. Baadaye anapiga simu hazina ambako anamwita mhesabu na karani wa idara ya fedha, mazungumzo yanafanyika na Brown Kwacha anasisitiza jambo mara baada ya kuwapatia milioni thelathini.Jengo la hazina linawaka moto, magari ya zinamamoto kutoka Halmashauri ya jiji, bandari na kikosi cha zimamoto kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mindule kinajumuika punde tu kujaribu kuzima moto ambapo milango na madirisha ya vioo vinateketezwa, Amani anasimama mbali na jengo huku akishindwa kuamini akionacho.Siku inayofuata Brown Kwacha na familia yake wanapanda ndege kwenda Geneva kwa ajili ya matibabu mara tu mahesabu ya wizara yanapotengenezwa na kutengemaa na Bunge kuridhia. Miezi mitatu baadaye Tino, mkewe na Amani wanakwenda uwanjani kumpokea Cheche na muuguzi wake kutoka kwenye tiba Glassgow, Uingereza. Tino namkewe wanamkumbatia Cheche machozi ya furaha yakiwabubujika.

UHAKIKI WA MAUDHUI

Dhamira Kuu: hali ngumu ya maisha

Joka la Mdimu ni riwaya inayoelezea ugumu wa maisha ambao jamii inakabiliana nao. Ugumu huu wa maisha kwa kiasi kikubwa unatokana na hali mbaya ya uchumi wa nchi. Watu masikini ni watu ambao wameathiriwa sana na ugumu wa maisha haya. Watu hawa wamekosa fedha za kujikimu katika maisha yao ya kila siku. Wananchi wanaishi katika maisha ya kijungujiko.Watu wa kawaida ndio wanaoumia na hali mbaya ya uchumi ambayo inatokana na siasa mbaya na uongozi mbaya, uhaba wa mafuta, mfumuko wa bei, rushwa, magendo, ufisadi na kutowajibika kwa viongozi wetu.Kutokana na kukosekana kwa mafuta, kunasababisha tatizo la usafiri kwa watu wa kawaida na kukosa mwanga kwenye nyumba zao wakati wa usiku, msanii [anasema (uk. 1)."Jiji la Mindule lilikabiliwa na uhaba mkubwa mno wa petroli, dizeli na mafuta ya taa,Nyumba nyingi zisizo na umeme zilibaki kiza usiku, maana mishumaa ilikuwa ghali naadimu kupatikana. Usafiri ulisimama isipokuwa kwa wale wachache waliojua mbinu zakupata petroli na dizeli"Kutokana na ugumu wa maisha, usafiri ni wa taabu na matatizo mengine mengi, watu wa tabaka la chini, hata kula kwao ni kwa taabu pia. Chakula chao kikuu ni kula mahindi ya njano kama anavyosema msanii (uk. 15 — 16)"Aibu hii. Miaka hamsini sasa tangu tumepata uhuru kila siku kula mahindi ya njano,"watu wa tabaka la chini wanaoishi mjini wanakumbana na matatizo mbalimbali yanayotokana na hali ngumu ya maisha. Kutokana na hali hii, hata kazi za kufanyahawachagui mradi tu wapate pesa ya kusukuma mbele maisha yao. Mfano Tino anafanyakazi ya kusuma kwama, Jinja Maloni anafanyakazi ya kuchimba makuburi na kupakuwa vyoo (uk. 46 — 50).Wakulima kwa upande wao vijijini nao wanakabiliwa na hii hali ngumu ya uchumi. Mazao ya biashara wanalima lakini hayawasaidii chochote kuinua hali zao za maisha, kwani wanaofaidi jasho la wakulima ni viongozi wachache. Matokeo ya yote hayo ni wakulima kuacha kulima mazao hayo ya biashara, msanii anasema."Ila kwa kifupi huko atakako watu wameacha kulima kahawa kabisa. Hawataki ""Kwa nini ?""Kipato kidogo, fedha yoteyenda serikalmi. Sijui tunaelewana? ""Naam !kutafutafedha za kigeni kwa ajili ya hao wakubwa""Halafu hakuna anayeziona! kulima walime wao, kufaidi wafaidi wengine ""Sasa wafanya nini?""Wanalima nyanya. fedha chapu chapu " (uk. 39 — 40)Wakati viongozi wanafaidi matunda ya mkulima, mkulima anapata matatizo makubwa sana kiasi cha kula mahindi ya njano, huku viongozi wako kwenye ziara nchi za nje na wala hawagusi mahindi ya njano kama anavyosema msanii anasema,"Lakini wao ziara za nje haziishi""Na wala mahindi ya njano hawayagusi""Basi waona" (uk 40)Hapa msanii anaonesha kuwa wakati viongozi wanatumia pesa nyingi kwa ziara ya nchi za nje, ziara hizo zinasababisha maumivu makubwa kwa watu wa tabaka la chini. Pesa ambazo zingetumika kuinulia uchumi wa nchi, viongozi wanazitumia kwa ziara zao za nje na mambo mengine ambayo hayana faida yoyote kwa jamii.Hali ngumu ya maisha vilevile imesababisha ubovu wa barabara zetu. Pesa kidogo zinazopatikana, badala ya kuzipeleka kwenye matengenezo ya barabara zetu zinatumika katika shughuli nyingine. Kwa upande mwingine serikali ikawa inasingizia haina hela ya kutengeneza barabara hizo, msanii anasema (uk. 81).Hakuna aliyejali kuyaziba mashimo hayo madogo au kama serikali ilivyodai, haikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kwa jinsi hiyo mashimo yaliendelea kuwa makubwa.Kwa ujumla, barabara ni nyenzo muhimu sana ya kulete maendeleao katika jamii, na ubovu wa barabara hasa unalete kero kwa watu wa kawaida ambao hutegemea barabara hizo kupata mahitaji muhimu.Vilevile msanii anaonesha kuwa kutokana na hali ngumu ya maisha watu wa vijijini nyumba zao na mavazi yao ni ya kusikitisha kama asemavyo msanii,"Hakukuwa na nyumba za maana isipokuwa kila baada ya mwendo wa nusu saawalitokea kwenye vijumba viwili, vitatu au vinne vilivyojengwa kwa suti za nyasi au udongomwekundu na kuezekwa kwa nyasi, Nje yake watoto wako uchi au kuvaa vibwende vya shukaza kishingoshingo, kaptura au vishati, waliangalia gari likipita" (uk 81).Hii ni hali ya watu wa kijijini, na huko mjini mambo ni hayohayo kwa watu watabaka la chini, maisha yao ya taabu, usafiri wa taabu watu hurundikwa kwenyemabasi kama mizigo na wengine huenda na kurudi kutoka kazini kwa mguukuepuka adha ya kusimama vituoni kwa muda mrefu bila ya uhakika wa kupata.usafiri (uk. 6-7). 'Kwa upande wa makazi, watu wa kawaida waliishi sehemu duni na chafu sana ukilinganisha na watu wenye pesa zao. Sehemu za makazi yao ilikuwa na uchafu ulevi, ufuska na ujambazi (uk. 26). Nyuimba zao ni mbovu na mvua ikinyesha inakuwa hatari tupu kwa watu wa tabaka la chini (uk. 29 — 30).Hospitalini vilevile kulikuwa na huduma mbovu kutokana na hali mbaya ya uchumi. Hakuna madawa halafu huduma zinazotolewa hazifai au zinatolewa kwa rushwa. Msanii anasema,"Huyu mtoto hawezi kupona hapa"Tino alisema kwa kubuhuti kikubwa""Eee!" Amani alikaa vizuri kwanini?""Hakuna tiba ya kufaa" (uk. 126).Wakati wenye pesa na viongozi wanakimbilia nje ya nchi kutibiwa, watu wa tabaka la chini (masikini) wanahangaika kupata huduma kwenye hospitali zetu na ili huduma itolewe lazima utoe chochote. Masikini wasio na chochote hukosa huduma hizo na matokeo yake ni vifo vingi vya watu masikini.Kwa ujumla, hali mbaya ya uchumi inawaandama watu wa kawaida, hawa ndio waathirika namba moja na hali hiyo mbaya ya uchumi. Watu wa kawaida wanakosa huduma muhimu kama vile chakula, sukari na vitu vingine muhimu kwa sababu ya kukosa pesa na vitu kuuzwa kwa bei ya juu. Haya yanaweza kuthibitishwa namazungumzo ya Zitto na Amani."Huko vijijini mbali Hapa vijijini sukari kilo shilingi mia tano utaweza? Zitto alibakiakimya na kumwacha Amani aendelee. "Haya hata wewe fikir viwanda zaidi ya vitanobado hakuna sukari" (uk, 16).Kwa viongozi ukosefu wa huduma muhimu kwa watu wa kawaida wanasingizia hawana fedha za kigeni za kununulia bidhaa muhimu. Hutumia visingizio tele, hikimara kile, eti dunia nzima ina matatizo ya uchumi na huu ni uongo mtupu kama asemavyo msanii,"Sio kweli. Tunazungumza na mabaharia kutoka nchi nyingine Afrika ambako hali simbaya. Uongo mtupu tu"(uk. 16)Matokeo ya hali mbaya ya uchumi ni kuwafanya watu wa kawaida (masikini) kujiingiza katika shughuli zisizo halali ili wajipatie fedha za kujikimu. Baadhi ya shughuli hizo haramu ni wizi, umalaya, ubakaji n.k. Kwa mfano, Tino alilazimika kuiba fedha benki ili aweze kumwokoa mwanae Cheche aliyekuwa ameumia kiuno chake (uk. 147 — 148). Pia mwanamke alivamiwa na kuporwa mkufu na hereni za dhahabu kama anavyosema msanii,"Washenzi, wamekata mkufu wangu wa dhahabu na kuchukua hereni zangu" (uk. 52).Katika kuonesha zaidi athari za hali mbaya ya uchumi, mwandishi anaonesha kuwa vijana wengi walijishughulisha katika shughuli za ukuwadi ili kupata pesa. Wanawake walifanya ufuska hata ndani ya gari bila aibu msanii anasema,"baada ya mwendo wa dakika karibu kumi, Amani alihisi kitu kinatokea kule nyuma. Bila kugeuka alitumia kiooo cha kuona nyuma; akaona abiria wale wamelaliana. Moyo ulimwenda kasi lakini hakusimama” (uk. 24)Hapa msanii anaonesha kuwa kutokana na hali ngumu ya maisha utu wa mtu hupotea, binadamu tunakuwa kama wanyama. Kitendo cha kufanya mapenzi mbele ya mwenzenu ni kinyume na utu kabisa na ni kikiuka maadili ya jamii kwa ujumla.Vilevile kutokana na ugumu wa maisha vijana wengi walijingiza katika uuzaji wabangi ili wapate pesa za kutatulia matatizo yao, msanii anasema,"Siku moja Amani alishuhudia kijana mmoja akimuuzia baharia mmoja kila moja ya bangi kwa dola mia tano za kimarekani". (uk. 25).Hali ngumu ya maisha imepoteza utu wa mwanadamu. Watu walifikia kufanya yote haya kwa sababu ya ugumu wa maisha tu. Hali mbaya ya uchumi imeathiri sanawatu wa kawaida (tabaka la chini).

Dhamira Nyinginezo

Rushwa katika famii

Rushwa ni fedha au kitu cha thamani ambacho mtu hupokea au kutoa ili kununua au kuuza huduma ya kijamii ambayo haikustahili kununuliwa kinyume na taratibu za utoaji wa huduma hiyo. Rushwa ni adui wa haki na maendeleo katika jamii yoyote. Mwandishi katika riwaya hii ameweza kubainisha tatizo la rushwa kamakichocheo cha hali mbaya (ngumu) ya maisha. Watoto wenye matatizo mbalimbali .hulazimika kutumia raslimali zao ili kuhonga watumishi wa umma ili kupata huduma au upendeleo fulani. Raslimali hizi zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo kama vile elimu, biashara, kilimo ambapo vingeweza kuinua hali ya uchumi: Haya yanathibitishwa katika kitabu pale mke wa Tino anaposema, ' haya, mjini tulikaa siku mbili mpaka tukapata tiketi za hongo, moja shilingi alfu nne. "..(uk. 71)Msomaji anaweza kuona namna rushwa ilivyoenea hadi katika sekta ya usafiri; watu wanaingia katika gharama ambazo si za lazima. Katika kushadidia kuhusu rushwa mwandishi anamwonyesha Amani namna anavyompa ofa daktari Mikwala ili amuandikie cheti kwenda Uingereza kwa matibabu. Mwandishi anasema,"Mazungumzo machache yaliendelea mpaka pale Amani alipokusudia kulivunja barazakwa kusema, Daktari nashukuru sana. Ngoja nikuache: Akachom*oa kitita cha noti nakumkabidhi." ...(uk. 133)Kwa upande mwingine Brown Kwacha anapokea rushwa ili aweze kuwahudumia wageni wake. Kwanza alipokea rushwa toka kwa Bhanj kama anavyosema msanii,"Sikia nakwisaveka dola laki moja ndani ya akaunti yako Genea"(uk. 92). Kitendo cha Brown Kwacha kupokea rushwa ni kinyume na maadili ya uongozi na hawa wanarudisha nyumba maendeleo ya jamii.Vilevile Brown Kwacha aliomba rushwa ili aweze kumwidhinishia fedha za kigeni Cheche ili akatibiwe ulaya, msanii anasema,"Anataka laki tatu ndipo aidhinishe kutolewa fedha za kigeni""Laki tatu?"(uk 141)Kwa upande mwingine Brown Kwacha alitoa rushwa kwa maofisa wa ardhi ili apate kiwanja cha kujengea nyumba (uk. 97).Kwa ujumla, kutoa au kupokea rushwa ni kosa la jinai: Jamii inapaswa kupiga vita rushwa kwani husababisha watu kukosa haki zao. Mbaya zaidi ni kwamba rushwa hufanya maisha ya watu kuwa duni zaidi na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Urasimu

Hii ni dhamira nyingine inayoelezea ugumu wa maisha katika jamii yetu. Ukiritimba wa viongozi katika kuhudumia wananchi umekuwa ukikatisha tamaa wananchi. Milolongo ya mambo ya kirasimu ndiyo chanzo cha ushawishi. Urasimu ni kikwazo kikubwa cha maendeleo na hivyo hufanya maisha ya watu kuwa magumu.Mfano mzuri tunaweza kuuona katika riwaya hii ya Joka la Mdimu ambapo kijana Cheche baada ya kuumia kiuno katika kujiandaa na sherehe ya uhuru. Anashindwa kupata huduma haraka kwa sababu za urasimu. Sababu mbalimbali zinatolewa kama vile serikali haina fedha za kigeni, kwenda bila ahadi n.k. kwa mfano, Amani anamwambia Brown Kwacha,"Mimi nimeletwa na shida ya mtoto wa ndugu yangu ambaye amekataliwa kupewa fedha za kigeni za kwenda kutibiwa Uingereza" (uk. 138). Brown Kwacha aliuliza,"Wajuaje kama amekatatiwa? . . .Siyo kakatiliwa nchi haina fedha za kigeni. ...... umechagua wakati mbaya wa kuzungumzia jambo hilo. Tafuta wakatimwingine"Kunapokuwa na viongozi wa aina hii wanaokumbatia urasimu ni kikwazo cha maendeleo na ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha katika jamii.

Kutowajibika

Hii ni dhamira ambayo inamulika viongozi wazembe ambao wamepewa dhamana na wananchi ili watumikie taifa lao. Kuna baadhi ya viongozi wameshindwa kutambua wajibu wao katika ofisi walizokabidhiwa badala yake ofisi hizi za umma wamegeuza kuwa miradi yao na kushindwa kuwatumikia wananchi.Mfano mzuri ni Brown Kwacha, Mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni aligeuza ofisi ya urnma kuwa sehemu ya kufanya ufuska, biashara haramu na kushindwa kuhudumia wananchi. Mwandishi anasema;"Broom Kwacha alikuwa kinyonga...Nyendo zake nyingi zilitiliwa shaka" (uk. 88).Katika kuonesha kuwa Brown Kwacha hakuweza kutumikia ofisi yake ipasavyo,mwandishi anasema."Katibu wa Brown Kwacha alimtazama mkuu wake wa kazi akastaajabu namna alivyoweza kukaidi kuwakudumia wengine na vile alivyolainika mbele ya wasichana." (uk. 94).Kwa ujumla viongozi wa namna hii ni wasaliti na kushindwa kuwajibika kwa jamii yao ni tatizo linalochangia wananchi wakose msaada na kuona maisha kuwa magumu bila sababu za msingi. Kama viongozi wangewajibika ipasavyo kero za wananchi zingetatuliwa na maisha ya wananchi yangekuwa bora.

Nafasi ya mwanamke katika jamii

Mwandishi anaweza kuonesha kuwa wanawake ni watu wanaoumia zaidi katika jamii. Mwandishi ameonesha kuwa wanawake wananyanyasika kutokana na mfumo mbaya wa maisha uliopo katika jamii kama ilivyo kwa watu wengine. Wanawake watabaka la chini waliathirika na ugumu wa rnaisha kama ilivyo watu wengine wa tabaka la chini.Wanawake pia waliathirika na mfumo dume ambao uliwapa fursa zaidi wanaume na huku ukiwadidimiza wanawake. Wanawake katika mfumo dume wananafasi zifuatazo:

  1. Wanawake ni wazazi na walezi: Mfano mzuri ni wema (mke wa Tino) alikuwa mama mzazi wa watoto watatu ambao ni Cheche, Tabu na Subira. Aliwazaa na kuwalea wote. (uk. 69). Vilevile mke wa Brown Kwacha alikuwa mama mzazi wa watoto watatu ambao aliwalea wakati wote (uk. 103).
  2. Mwanamke pia amechorwa kama chombo cha starehe. Wanawake walichukuliwa kama chombo cha kuwastarehesha wanaume pindi wanapojisikia.

Mfano mzuri ni wale wanaume mabaharia walivyokuwa wakiwatumia wanawake kama chombo cha kujistarehesha. Mfano mwingine., unamhusu mkurugenzi Brown Kwacha aliyekuwa anabadilisha wanawake kama nguo kwa lengo la kujistarehesha. Mwandishi anasema,"Maana kadtri alivyotembea na mwanamke mmoja mzuri ndivyo ashkiyake alichochewa akitamani tena na tena. Alishafumaniwa na mkewe, nyumbani na hata ofisini, Sio hivyo tu, alikwishavunja ahadi kadhaa za wachumba. Tayari alifumaniwa na wanaume akitembea na wake zao " (uk. 91)

  1. Mwanamke amechorwa kama kiumbe duni asiyeweza kutoa mchango wowote wa mawazo. Haya tunayaona kwa Brown Kwacha ambaye hakuwa akimshirlkisha mke wake katika maamuzi (uk. 97).
  2. Mwanamke amechorwa kama mtu jasiri na mwenye msimanio. mfano Pamela ambaye aliviruka vihunzi vyote vya Brown Kwacha na Kwacha alistajabia na akimshirlkisha mke wake katika maamuzi (uk. 97).
  3. Mwanamke amechorwa kama mtu jasiri na mwenye msimanio. mfano Pamela ambaye aliviruka vihunzi vyote vya Brown Kwacha na Kwacha alistajabia na tabia hiyo ya Pamela. Brown Kwacha alimtaka Pamela kimapenzi kwa vishawishi vya pesa lakini Pamela alionesha msimamo na ujasiri akamkataa Kwacha (uk. 96).

Kwa ujumla, mwanamke amedidimizwa sana katika riwaya hii. Amechorwa kuwa ni muhanga wa kila aina ya uonevu, unyonyaji na unyanyasaji.

Mapenzi na Ndoa

Hii ni dhamira ambayo mwandishi ameishughulikia katika riwaya hii. Mwandishi ameonesha (mapenzi ya aina mbili mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo).Mapenzi ya kweli ni kati ya Tino na Amani. Hawa walikuwa marafiki wa kweli na wakisaidiana katika shida na raha. Amani alimsaidia sana Tino katika harakati zake za kumtibu mtoto wake Cheche (uk 77). Vilevile Amani alimsaidia Tino kwenda kuiba pesa benki ili wampeleke mtoto wake Cheche ulaya kutibiwa (uk. 147 _ 148).Mapenzi mengine ya kweli yako kati. ya Tino na Jinja Maloni. Hawa walipendana hasa na ndio maana Tino aliamua kuishi nyumbani kwake na Jinja kwa ajili ya ku*msaidia asiathirike sana na mji.Mapenzi kati ya Zitto , Amani na Tino yalikuwa ya kweli hawa walipendana sana na walishirikiana katika ulevi waoMapenzi mengine ya kweli ni ya Tino kwa watoto wake hasa Cheche. Tino pamoja na kwamba hakuwa na kitu zaidi yakusukuma kwama aliwapenda sana watoto wake. Aliwapa zawadi za kila aina hasa wakati wa sikukuu. Ni kutokana namapenzi ya kweli kwa mtoto wake, Tino alilazimika kwenda kuiba fedha benki ili akamtibu mtoto wake Cheche ulaya.Kwa upande wa mapenzi ya uongo ni kati ya Brown Kwacha na wanawake zake kama vile Josephine, Leila na wengine wengi. Mapenzi ya hawa yaliegemea katika pesa na hayakuwa mapenzi ya kweli.Mapenzi mengine ya uongo ni kati ya Brown Kwacha kwa watoto wake. Brown Kwacha hakuwa na mapenzi na watoto wake, ndio maana walimuogopa sana na ilifikia hatua walishindwa hata kumuomba kitu.Kuhusu ndoa nazo msanii ameainisha aina mbili za ndoa ya kweli na ya oungo. ndoa ya kweli ni kati ya Tino na Wema. Hawa walikuwa na mapenzi ya dhati katika ndoa yao. Walishirikiana kulea watoto wao watatu na pale wapotofautiana wajirekebisha, mwandishi anasema;"Tino alioa akiwa na umri ma miaka ishirini tu, Wema alikuwa mke ndugu, yaani mtoto wa mjomba wake. Mapenzi makubwa baina yao yalikamilishwa na udugu" (uk. 71)Kwa upande wa ndoa ya uongo ni kati ya Brown Kwacha na mke wake. Brown Kwacha hakumpenda mke wake ndio maana alibadilisha wanawake kama nguo na bila kumjali mke wake . Nyumbani hakuwa na raha na mkewe wala watoto wake, kila siku visingizio (uk. 91). Kutokana na kutokuwa na uaminifu katika ndoa yake alifikia hatua akawa anawaleta wanawake wa nje hata nyumbani kwake kama anavyosema msanii,"Mke wake Kwacha aliwafumania nyumbani kwake wamejibwaga kitandani kalamu ikiandika"(uk. 94).Ndoa za uongo au kukosa uaminifu katika ndoa huwa ni chanzo cha mateso ndani ya nyumba na kukosekana kwa amani ndani ya familia, mwandishi anasema,"Baina yake na mumewe palikuwa, na mkato mithiliya wembe: Vigumu kuonekana kwa macho ila kwa madhara yake, Alikonda akajipa moyo, akarudisha hali yake, akakonda tena na tena" (uk. 104).Kwa ujumla, kukosa uaminifu katika ndoa huvuruga amani na utulivu kati ya mke na mume na matokeo yake ni kusambaratika kwa ndoa hiyo.

Uhujumu uchumi na magendo

Uhujumu uchumi na magendo ni dhamira nyingine inayojadiliwa katika riwaya hii ya Joka la mdimu. Uhujumu uchumi na magendo ni tatizo linalokwamisha maendeleo ya nchi na hali ngumu ya maisha kwa watu wa tabaka la chini. Msanii anaonesha kuwa wahujumu uchumi wa nchi wengi ni viongozi na wafanyabiashara. Uhujumu uchumi na magendo umekuwa ukisababisha taifa kukosa mapato halali na matokeo yake mapato hayo yanaangukia mikononi mwa wachache.Katika riwaya hii, msanii anaonesha kuwa viongozi wa serikali wako mstari wa mbele katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa kumeza nyara za serikali kwa magendo na hivyo kulikosesha taifa mapato yake. Mkurugenzi Brown Kwacha anashirikana na wafanyabiashara kusafirisha pembe za ndovu nje ya nchi kwa magendo, msanii anasema,"Kwacha akamnong'oneza, "Lakini safari hii nina Consignment kubwa karibu pembe mia tatu hivyo angalia sana" (uk. 93).Brown Kwacha kama kiongozi wa umma anaihujumu nchi yake kwa kushirikiana na wafanyabiashara. Vilevile Brown Kwacha alikuwa anawinda wanyama kwa siri na kupata pembe za ndovu na faru kwa faida yake na hivyo kuhujumu uchumi wa nchi (uk. 106).Vilevile Brown Kwacha alishirikiana na majangili (wawindaji haramu) kuhujumu uchumi wa nchi. Brown aliwajiri watu ambao waliwinda wanyama nakupata Pembe zake kwa ajili ya kuuza nje kwa faida yake. Brown Kwacha alinunua pembe hizo kwa wawindaji wake kama asemavyo msanii,"Sawa,ziko pembe ishirini za faru na sitini za ndovu " (uk. 119).Kutokana na kitendo hiki cha akina Brown Kwacha na wawindaji wengine, wanyama kama ndovu na faru wanapungua mno kutokana na kuwindwa kila siku na wawindandaji haramu, Vilevile Brown Kwacha aliwasaidia wawindaji haramu bunduki, risasi pamoja na darubini ili waweze kuraisisha kazi zao za uwindaji (uk. 120- 121). Huu wote ni uhujumu uchumi wa nchi na watu kama Brown Kwacha wapo katika jamii yetu. Ili tuinue uchumi wa nchi yetu lazima tuwapige vita watu kama hawaBrown Kwacha angekuwa mfano wa viongozi wa kupiga vita biashara haramu, lakini ndiye kinara wa biashara hizo. Aliweza kukodi majangili ili kuwinda ndovu wetu ambao wangetumika katika utalii ambao ungetuingizia fedha za kigeni. Nchi inahitaji fedha hizi kwa shughuli za maendeleoKwa upande mwingine, msanii anaonesha kuwa watu wengi wanafanya biashara za magendo na hivyo kilikosesha taifa fedha ambazo zingetumika kuinulia uchumi wa nchi. Mfano mzuri tuna Kashogi aliyefanya biashara za magendo za kuuza mafuta na hivyo kulikosesha taifa mapato yake (uk. 17). Hata kwenye vituo vya mafuta wafanyakazi waliuza mafuta kwa magendo na kwa bei kubwa (uk. 11).Uhujumu uchumi wa wanchi magendo ni vitu vya hatari sana katika uchumi wa nchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla, Ni lazima vikomeshwe ili kupunguza ugumu wa maisha.Vilevile kuungua kwa jengo la hazina ni sehemu ya uhujumu uchumi. Brown Kwacha alihusika moja kwa moja na uchomaji wa jengo hilo, kwani kuchomwa kwa jengo hilo , kulisaidia kuteketeza nyaraka muhimu ambazo zingemsababishia matatizo katika kazi yake (uk. 156 — 157) kitendo cha Brown Kwacha kwenda Ulaya baada ya kuungua jengo hilo kinadhihirisha jinsi anavyohujumu uchumi wa nchi. Hata mahesabu ya wizara yaliyotengenezwa na kupelekwa bungeni yalikuwa ni batili kwa sababu yalikuwa ya uongo mtupu.

Matabaka

Matabaka ni ile hali ya jamii moja ya watu kuwa na tofauti kubwa kwa misingi ya kiuchumi na kielimu. Mwandishi ameonesha kuwa mfano wa maisha ya watu wa Mindule na miji iliyoko jirani umechangia sana kutokuwepo kwa usawa. Mfumo wa maisha umepelekea kuwa katika makundi makuu mawili; Kundi la walionacho (Matajiri) ambalo linawakilishwa na watu kama Bhanj, Brown Kwacha na Mawaziri wa Serikali. Kundi la pili ni lile la watu wasiokua nacho ambacho kinawakilishwa na Tino.Kwa ujumla mfumo wa maisha na kutowajibika kwa serikali kwa watu wake wote kumetoa mwanya kwa matajiri kama Brown Kwacha kujirimbikizia mali nyingi kwa njia za magendo, wizi na rushwa. Matajiri hawa wanaishi maisha ya kifahari kwa kujirimbikizia fedha za kifani na kujenga majumba ya kifahari: Kwa mfano katika (uk 103-104) mwandishi anasema hivi kuhusu nyumba ya Brown,"Ilisimama na kuzibeba nyumba zote za jirani na hapo kwa haiba yake, na bwawa lake la kuogelea".Wakati hiyo ndiyo hali halisi ya maisha ya watu wa tabaka la juu, Mwandishi anaonesha kuwa katika jamii hiyo kulikuwa na watu waliishi maisha ya dhiki na uf*ckara uliotopea mathalani, Tino aliishi katika nyumba iliyokuwa ikivuja (uk 29) na watoto hawakuwa na nguo za kuwasitiri (uk 83).Hivyo basi ni muhimu kwa serikali kuondoa tofauti hizo kwa kutubadilisha mfano wa maisha utakaosaidia wote kuishi katika maisha bora.

Ufisadi

Hii ni hali ya watu walio katika nyadhifa kutumia fursa ya madaraka kujitajirisha kwa kutumia rasilimali za nchi katika miradi yao binafsi.Mwandishi anaona kuwa ufisadi wa viongozi umefanya wananchi waendelee kubebeshwa mizigo ambayo si ya lazima na hivyo maisha kuwa magumu kwa wananchi Mfano mzuri wa viongozi ambaye ni fisadi ni Brown Kwacha. Aliweza kujenga nyumba kubwa mbili za gharama kubwa mwandishi anasema,"Gharama ya nyumba iliyokuwa ijengwe na Wafaransa ilikuwa shilingi milioni mia mbili na nusu na ile nyingine milioni mia tatu. Vifaa vyote, isipokuwa mbao na saruji vilikuwa vitoke nje."Hizi fedha nyingi sana. Kwa mshahara wake tu asingeweza kujenga. Biashara za magendo, pesa za kigeni katika ofisi yake na rushwa ndivyo vyanzo vikuu vya fedha. za ujenzi wa nyumba yake.Hali hii ni hatari kwa nchi, kwani hizo fedha za kigeni wanazodai hakuna hata kupeleka wagonjwa hospitali kutibiwa ndizo zinatumika kununulia mahitaji yao. Maslahi ya taifa lazima yapewe kipaumbele. Ubinafsi wa viongozi unakwamisha maendeleo ya nchi na kufanya maisha ya watu kuzidi kuwa magumu zaidi.

Migogoro

Migogoro kadhaa imejitokeza katika riwaya hii.

  • Mgogoro wa kwanza ni kati ya makundi wawili ambao walipigana kwa kugombania kushusha magogo katika gari (uk. 34).
  • Mgogoro mwingine ni kati ya Jinja na vibaka ambao walikuwa wanambaka mama mmoja na kukwapua mkufu na hereni za mama huyo. Alipotaka kumuokoa huyo mama walikuja juu na kuanza kupigana naye. Jinja alifanikiwa kumuokoa yule mama (uk. 51- 52).
  • Mgogoro wa tatu ni wa kinafsia uliokuwa ndani ya Tino. Aliwaza namna ya kupata fedha ya kumtibu mwanae Cheche. Anaposhauriwa kwenda kupora fedha alisifia. Alishindwa kuamua kama aendelee na mpango huo lakini alihofu; alipowaza namna mwanae anavyoteseka aliumia moyo. Mwisho aliamua kwenda kupora fedha benki kiasi cha milioni 20 na kufanikiwa kwenda kumtibu Uingereza mwanae. (uk. 143 -148).
  • Mgogoro wa nne ni kati ya katibu mkuu wa Wizara ya Mila na Utamaduni na kijana ambao walipigana katika siku ya uzinduzi wa nyumba ya Brown Kwacha,Walikuwa wanagombania msichana aitwae Esther, (uk. 102).
  • Mgogoro mwingine ni kati ya mke wa Brown, Brown na Josephine. Mke wa Brown Kwacha alimfumania Brown Kwacha akiwa anfanya mapenzi na Josephine. Mke wa Brown Kwacha alimpiga Josephine hadi mdomo wa chini ukapasuka (uk 94).

Kwa ujumla, migogoro yote hii imetumika kusukuma riwaya mbele na kujaribu kuonesha chanzo cha matatizo ambayo yamejadiliwa kama dhamira.Hata hivyo mwandishi anautoa masuluhisho ambayo yanaongeza uhalifu katika jamii, kwa mfano kujihusisha na dawa za kulevya, umalaya, kupigana au kuiba benki si masuluhisho bora kuna haja waandishi kutoa masuluhisho endelevu katika jamii.

Ujumbe wa Mwandishi

Mwandishi wa riwaya hii ametoa maadili au mafunzo kadhaa kwa jamii. Mtu anaposoma riwaya hii anapata mafunzo yafuatayo;

  • Ufisadi wa viongozi ni uhalifu mkubwa ambao unamadhara makubwa katika maisha ya wananchi walio wengi. Jamii haina budi kupiga vita ufisadi ili raslimali zao ziwanufaishe wanajamii wote.
  • Rushwa ni adui wa haki., penye rushwa haki hujitenga. Rushwa ni ndugu mkubwa wa ufisadi. Hivyo, jamii lazima ipambane na vitendo vyote vinavyozuia haki isitendeke katika jamii.
  • Mapenzi ya dhati ndani ya jamii ni muhimu sana kwa wanandoa, marafiki na familia hawana budi kuwa na mapenzi ya dhati ili kudumisha amani miongoni mwao.
  • Jamii inapaswa kubadili mfumo wa maisha unaowakandamiza wanawake ili wasiendelee kuwa chombo duni, tegemezi au chombo cha starehe.

Mtazamo wa Mwandishi

Mwandishi Abdalah J. Safari ana mtazamo wa kiyakinifu. Mwandishi ameweza kuainishi kero mbalimbali walizonazo wananchi. Mwandishi ameeleza uozo uliomo ndani ya jamii bila woga na namna wakubwa wanavyohusika na uozo huo. Mwandishi anaonekana anawanyoshea kidole viongozi kuwa ndiyo chanzo cha maisha magumu kwani wananchi wa kawaida wanajituma kurekebisha maisha yao duni lakini kikwazo kimekuwa ni viongozi ambao ni mafisadi na warasimu.Jamii inapaswa kubadili mfumo wa maisha unaowakandamiza wanawake ili wasiendelee kuwa chombo duni, tegemezi au chombo cha starehe.

Falsafa ya Mwandishi

Mwandishi anaelekea kuamini kuwa matatizo makubwa yanayojitokeza katika jamii yanasababishwa na kutowajibika kwa viongozi, urasimu na ufisadi ndio kikwazo

FANI

Muundo:

Riwaya ya Joka la Mdimu ina jumla ya sura kumi (10) ambazo amezipa majina kutokana na majina ya wahusika, mahali na matukio yanayobeba kisa kizima cha hadithi hiyo katika sura husika. Kila kisa amekieleza kwa masimulizi ya msago, maisha ya kila mtu na miji kuelezea moja kwa moja visa na matukio unaweza kuandika kwa muhtasari kama ilivyooneshwa kwenye sehemu ya pitio la kitabu.

Mtindo

Riwaya hii ya Joka la Mdimu ipo katika mtindo wa masimulizi. Nafsi ya tatu ndiyo imetawala kwa kiasi kikubwa, japokuwa kuna matumizi ya nafsi ya kwanza na pili pia. Dayolojia imetumika kiasi kidogo tu. Mwandishi amefanya hivyo ili kuweka uhalisia wa mazungumzo baina ya wahusika. Mwandishi pia ameweza kutumia nyimbo katika riwaya hii. Wimbo wa Chaupele upo."Chaupele mpenzi hayo usemayo Kama ni maradhi yapeleke kwa daktariWanambia niliache rumba, na mimi sikuzoeaSitaweza kuliacha rumba kwa sababu yako,Kama wampenda nenda kwa baba,Utoe mapesa, ndipo urudi unioe"(uk. 70 - 71).

Wahusika

Amani

Huyu ni mhusika mkuu. Ni dereva wa taxi. Ni kijana mchapa kazi, ana huruma, ana hekima na busara. Anafaa kuigwa na jamii.

Brown Kwacha

Huyu ni mhusika msaidizi. Ni mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni, Ni malaya, Si mtu adilifu, Ni fisadi, Anapenda rushwa, Anafanya biashara za magendo na Hafai kuigwa.

Tino

Huyu ni mhusika mkuu msaidizi. Ni mvuta kwama. Ni baba wa watoto watatu. Ni jasiri. Ni mchapa kazi. Mwanamichezo. Anafaa kuigwa.

Jinja Maloni

Ana upendo, mlevi, mkakamavu, si muoga. Hafai kuigwa.

Daktari Mikwala

Ni daktari bingwa wa mifupa. Ni mlevi, anapenda rushwa. Hafai kuigwa.

Shiraz Bhanj

Ni mfanyabiashara. Mtoa rushwa. Ni rafiki yake Brown Kwacha. Hafai kuigwa.

Zitto

Ni mfanyakazi wa bandari. Ni rafiki yake Amani na Tino. Ni mtu wa kipato cha chini. Ni mwanamichezo.

Cheche

Ni mtoto wa kiume wa Tino. Ni mvulana anayesoma. Ndiye aliyeumia kiuno wakati wa michezo ya kusherekea uhuru wa nchi. Ni mtoto mwenye tabia njema. Ni mcheshi, mdadisi na mwanamichexo. Alipendwa sana na watu.Wahusika wengine ni Leila, Josephina, Pamela. Hawa wamejitokeza kama wahusika ambao wamekuwa marafiki wa kike wa Brown Kwacha.

Matumiz ya lugha

Lugha iliyotumika ni ya kawaida iliyoshehenezwa tamthilia za semi na mbinu nyingine zaKisanaa.

Misemo

Asiye na bahati habahatishi (uk, 10).Tandu kwenda nyuma na mbele ndiyo hulka yake. (uk. 25).Asiyezika hazikwi(uk. 48),Mmetupajongoo na mtiwe (uk. 64)

Methali

Asilolijua mtu ni usiku wa giza (uk. 77)Ukiona mwenzio ananyolewa, tia maji (uk, 83)Mtaka waridi sharti avumilie miiba (uk, 98)Biashara haigombi (uk. 99)

Matumizi ya Lugha Nyingine

• Mwandishi ameigiza maneno ya Kiingereza sehemu mbalimbali.Kwa mfano:- Missions to seamen please, (uk. 24). - -- Hey men will you pay extra dollars (uk. 24).* Matumizi ya lugha ya Kiarabu. Kwa mfano:"lnna Lillahi wa Inna Ilahi Rajiunna! (uk. 41).

Tamathali za Semi

Tashibiha

  • Zalpher 6 ile iliunguruma kama simba dume aliyeghadhibishwa. (uk. 9).
  • Wote walikimbilia kula wakiminyana kufa au kupona kama kaa wanavyogombea mavi ya mvuvi. (uk. 21).
  • Maduka makubwa yalichipua mithili ya uyoga. (uk. 26).
  • Miguu yake ilikazana mithili ya upinde uliotaka kufyatuliwa (uk. 33).

Tashihisi

Utumbo ulimlaumu (uk. 12).Mvua ikarindima kwa kiburi na kuviadhibu vibati vibovu (uk. 27).Lakini hata fikra nazo zilikuwa kama zimempiga chenga. (uk. 4).SitiariSote ni kobe (uk, 72).Sarahange wetu mboga kweli siku hizi (uk. 15).

Mbinu Nyingine za Kisanaa

Onomatopoea/ Tanakali Sauti".

Mfano:-

  1. Saa mezani iliendelea kugonga, "ta ta ta".
  2. Akazungusha ufunguo wa gari lake kutaka kuliwasha lakini ikatokea sauti kali fupi, "ta nye nye".

Takriri

Funga, shinda! funga, shinda ! saut za mashabiki zikalindima tena (uk. 56).Shinda! shinda! shinda!kibanda kilitememeka tena (uk. 55).Shetani! oyee! Shetani! oyee! Shetani chinja! (uk. 58).

Mandhari

Riwaya hii imejengwa katika mazingira ya mjini. Mwandishi ametumia majina ya miji ya Mindule, Sega na Boko ambayo ipo nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam.Mandhari haya yanaweza kugusa nchi zote zinazoendelea ambapo kuna hali ngumu ya uchumi na matatizo ya ufisadi na urasimu.

Jina la kitabu

Joka la Mdimu ni jina la kitabu ambalo linajengwa kwa lugha ya picha. Joka la Mdimu ni aina ya nyoka ambaye huishi katika miti ya kijani. Joka hili hupendelea kuishi katika minyaa na midimu. Nyoka huyu huwa na rangi ya kijani ambapo si rahisi kumuona kwa macho kwani hufanana sana na matawi ya mti aliyomo. Nyoka huyu ni hatari sana kwa maisha ya watu.Joka la Mdimu limetumika kuwakilisha viongozi hatari kama nyoka huyu. Viongozi wote mafisadi kama ilivyo kwa Brown Kwacha wamelinganishwa na joka hili la mdimu.Kwa ujumla jina la kitabu linasadifu yote yaliyomo ndani ya kitabu, kwani kitabu kizima kinazungumzia mafisadi na walanguzi, wahujumu uchumi, watoa rushwa na wapokea rushwa na wanaofanya magendo, Hawa ndio majoka wenyewe. Wahusika hawa wanaishi nasi na kufanana nasi lakini undani wa maisha yao ni hatari sana kama ilivyo kwa joka la mdimu.

Kufaulu na Kutofaulu

Kufaulu

Kimaudhui mwandishi amefaulu kuelezea matatizo yanayoikabili jamii. Ameeleza kwa uwazi bila kuficha namna maisha ya watu wa tabaka la chini yalivyo magumu wakati viongozi na wafanyabiashara wanafurahia maisha. Ameeleza kwa dhati matatizo ya uhujumu uchumi, urasimu na ufisadi yanavyokuwa tatizo katika maendeleo,Kifani mwandishi amefaulu kutumia lugha ambayo amewapa wahusika kulingana na uhusika wao. Ametumia tamathali za semi ambazo zinabeba dhamira ya mwandishi.

Kutofaulu

Mwandishi ameshindwa kuonesha masuluhisho ya matatizo husika. Hata pale anapotoa masuluhisho ya matatizo yanakuwa ni ya kihalifu zaidi. Kwa mfano, mahesabu yanapokuwa mabaya., Brown Kwacha anatatua kwa kufunga wahasibu wake watengeneze mahesabu na bunge linakubali. Au Tino anapokosa fedha za kumuuguza mwanae anaenda kupora fedha benki na hakamatwi. Mwandishi anaonekana kuhalalisha matumizi ya nguvu za kihalifu kutatua matatizo katika jamii. Lingekuwa jambo la busara kama kungekuwa na hatua za uwajibishwaji watu katika kuondoa uozo uliomo katika jamii.

UHAKIKI WA RIWAYA YA JOKA LA MDIMU (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Horacio Brakus JD

Last Updated:

Views: 6177

Rating: 4 / 5 (51 voted)

Reviews: 90% of readers found this page helpful

Author information

Name: Horacio Brakus JD

Birthday: 1999-08-21

Address: Apt. 524 43384 Minnie Prairie, South Edda, MA 62804

Phone: +5931039998219

Job: Sales Strategist

Hobby: Sculling, Kitesurfing, Orienteering, Painting, Computer programming, Creative writing, Scuba diving

Introduction: My name is Horacio Brakus JD, I am a lively, splendid, jolly, vivacious, vast, cheerful, agreeable person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.